Je vita vinasambaa?

Milipuko ya ajabu katika Transnistria, jimbo lililojitenga linalodhibitiwa na Urusi katika Moldova linalopakana na Ukraine, imeibua hofu kwamba vita vya Ukraine huenda vinasambaa katika maeneo mengine zaidi.

Maafisa wa eneo hilo lililojitenga wanasema Waukraine "waliojipenyeza " walihusika na milipuko hiyo. Lakini Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amevilaumu vikosi maalumu vya Urusi kuhusika na shambulio hilo.

Urusi inasema inahofu. Ina wanajeshi takriban 1,500 troops katika Transnistria.

Afisa mmoja amesema watu wanaozungumza Kirusi katika Moldova wanadhulumiw.

Hiki ni kisingizio sawa na kilichotumiwa kuhalalisha uvamizi wa Ukraine.

Katika kipindi cha siku mbili zilizopita ,maafisa katika Transnistria walisema vilipuzi vililenga:

Hakuja majeruhi walioripotiwa, lakini tahadhari ya "kupambana na ugaidi " imetangazwa sasa, ikimaanisha usalama umeimarishwa katika eneo, ambalo lilijitenga kutoka Moldova katika vita vya muda mfupi vya mwaka 1992.

Maafisa wa Transnistria walisema kuwa watu watatu waliopenya na kuingia katika eneo hilo kutoka Ukraine walishambulia makao makuu ya usalama kwa kifaa kinachofyatua gurunedi. Dai hilo bado halijathibitishw.

Ofisi ya Rais nchini Urusi - Kremlin inasema inatazama hali kwa karibu na "ni jambo linalotia hofu".

Katika mji mkuu Kyiv, Rais Zelensky alikuwa wazi kwamba Urusi ilikuwa nyuma ya shambulio hilo, na kuongeza kuwa: "Lengo linaeleweka wazi -kuyumbisha hali katika jimbo , kuitisha Moldova.

Walionyesha kuwa iwapo Moldovainaunga mkono Ukraine, kutakuwa na fulani ."

"Lakini tunafahamu uwezo wao, vikosi vya silaha vya Ukraine viko tayari kwa hili na haviwaogopi ," alisema Rais Zelensky Jumanne.

Shabulio katika Transnistria linaweza kuiyumbisha Moldova na kufungua eneo jipya la vita. Odesa, mji muhimu wa bandari wa Ukraine, upo mashariki mwa Transnistria.

Kama Urusi itajiimarisha katika Transnistria, inaweza hatimaye kusonga katika mji wa Odesa kutoka magharibi.

Kusonga mbele kwa majeshi yake katika mji huo yakitokea mashariki kulizuiwa na vikosi vya Ukraine. Hilo litakuwa ni kuugeuza mwelekeo wa kivita wa vikosi vya Ukraine ambavyo tayari vimesonga mbele sana.

Ijumaa jenerali wa ngazi ya juu wa Urusi, Rustam Minnekayev, alisema "udhibiti wa kusini mwa Ukraine ni njia nyingine ya kufika Transnistria, ambako pia kuna matukio ya kudhulumiwa kwa watu wanaozungumza lugha ya Kirusi ".

Rais Vladimir Putinameahidi "kulinda" jamii za Warusi katika Jamuhuri zilizojitenga zilizokuwa katika Muungano wa Usoviet . Hayo yalikuwa madai yake yaliyosababisha uvamizi wa Ukraine. Moldova ilikuwa katika Jamuhuri ya Usovieti zamani.

Leon mshirika wa karibu wa Moldova ni karibu ni Romania , lakini kinyume na Romania, Moldovahaiko katika Nato au Muungano wa Ulaya. Wamoldova wana paspoti za Romania na hufanya kazi katika Muungano wa Ulaya - EU.

Moldova ni moja ya matifa masikini zaidi ya Ulaya. Ni makao ya watu wanaozungumza lugha ya Ukraine. Imewachukua wakimbizi wa Ukraine zaidi ya 437,000 na ni nchi yenye jumla ya watu milioni 2.6 , idadi ambayo ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine yoyote ile yenye ukubwa wake.

Rais wa Moldova Maia Sandu anaunga mkono sana Muungano wa Ulaya, lakini mtangulizi wake Igor Dodon - ambaye bado ana wafuasi wengi wanaomuunga mkono-alikuwa anaunga mkono Urusi.

Moldova imepiga marufuku kuonyeshwa wazi kwa alama za kitambaa cha St George na Z zinazotambuliwa kama alama za utambulisho wa uvamizi wa kijeshi wa Urusi katika Ukraine.


Eneo lililojitenga la Transnistria - ni sehemu nyembamba ya ardhi inayopatikana katikati yam to Dniester na mpaka wa Ukraine - ambapo lilijitangazia uhuru wake kutoka Moldova mwaka 1990 - ingawa Jamii ya kimataifa utaifa wa wake.

Baada ya Vita kuu ya pili ya dunia, Moscow ilibuni taifa la awali la Jamuhuri ya Moldavia ya Usovieti ya kijamaa, kutoka katika jimbo linalozungumza lugha ya Kirusi la Dniester region, ambalo limekuwasemu ya Ukraine inayojitawala, na jimbo jirani la Bessarabia, ambalo limekuwa sehemu ya Romania kuanzia 1918 hadi 1940.

Lakini wakati Muungano wa Usovieti ulipovunjika, kuliibuka hali ya wasi wasi katika - jimbo la Dniester kuhusu kuongezeka kwa hisia za utaifa miongoni mwa Wamoldova na uwezekano wa kuiunganisha tena Moldova na Romania, nae neo hilo likajitangazia kujitenga tena.

Watu wapatao 700 waliuawa katika vita vya muda mfupi vya mpaka baina ya Moldova na Transnistria -mkataba wa kusitisha mapigano ulisainiwa mwaka 1992. Utekezwaji wa makubaliano ulisimamiwa na vikosi vya Urusi vilivyokuwa katika Transnistria.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii