Waislamu na wanajamii kwa ujumla
wametakiwa kuutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kubadili tabia kwa
kutenda yaliyo mema na kuyaendeleza hata baada ya kumalizika mfungo.
Rai
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni GF Truck
& Equipments LTD, Mehboob Karmali mara baada ya kufuturisha wadau
mbali mbali na wafanyakazi wa kampuni hiyo .
Alisema mara nyingi
mwezi huo umekuwa ukileta utulivu katika jamii, “Haijalishi ni kijana,
mzee, Muislamu na asiyekuwa mwislamu, ilimradi wengi hutulia na
kuuheshimu, hivyo ni vema kuendeleza yale mema hata katika nyakati
nyingine ili jamii iwe salama.
“Kipindi hiki pia ni vema kuwapa
wahitaji sadaka kwa kile kidogo tutakachojaaliwa kwa sababu tunazidiana
“alisema Karmali.Kwa upande wa mgeni mualikwa katika Iftari hiyo, Sheikh
wa msikiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Uingereza, Syed Ali
Raza Rizvi aliwasihi Waislamu hususani vijana kudumisha amani na upendo
baina yao.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa wafanyakazi wa
kampuni hiyo kufanya kazi huku wakimtanguliza Mungu ili wanapofanya
maamuzi yoyote yawe kwa faida ya kazi yao na Taifa kwa ujumla.
“Ukimtanguliza
Mungu katika kila jambo lazima utafanikiwa, ila ukiwajali wengine na
kuwahurumia utafanya maamuzi ya busara siku zote, hivyo tuyazingatie
haya ili kufikia mafanikio tunayoyakusudia”alisema Raza Rizvi.
Hii
ni kawaida kampuni ya GF Trucks & Equipemnts LTD, kujumuia na
wafanyakazi wake na wadau katika matukio mbalimbali ikiwamo kufuturisha
pamoja na kutoa misaada kwa yatima na wasiojiweza.
Kampuni hiyo inajishughulisha na uuzaji wa magari makubwa(trucks) na mitambo ya kutengenezea barabara.