TULIKUPENDA,
Tunakupenda na yote uliyofanya kwa nchi yetu vitaishi mioyoni mwetu, ni
kauli za watanzania wengi baada ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
kutangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Joseph Magufuli aliyefariki dunia jana katika hospitali ya Mzena Mkoani
Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa maradhi ya moyo.
Hayati John Pombe Magufuli (61)
anaingia katika orodha ya viongozi wakuu wa nchi barani Afrika
waliofariki wakiwa madarakani, Magufuli ameongoza kwa kuwa kipindi cha
2015/ hadi Machi 2021, huku akifa kwa Marathi ya Umeme wa Moyo ambapo
Marais wengine ni pamoja na;
Pierre Nkurunziza (64)
Alikuwa Rais wa nane wa Burundi na alihudumu kwa miaka 15 (Januari hadi Juni 2020) na alifariki dunia 2020 kwa mshtuko wa moyo.
Michael Sata (77)
Alikuwa
Rais wa Zambia aliyehudumu kama Waziri kwa miaka ya 1990's kabla ya
kuongoza taifa hilo kuanzia 2011 na alifariki dunia 2014 kwa maradhi
ambayo hayakutajwa.
Meles Zenawi (57)
Alikuwa
Waziri Mkuu wa pili wa Ethiopia kabla ya kupata nafasi ya kiti cha
urais na alifariki dunia 2012 nchini Ubelgiji kwa maradhi ambayo
hayakutajwa.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii