Kila mwaka, familia nchini Marekani zinawaleta majumbani maelfu ya watoto wanaotoka ndani na nje ya nchi kuwalea. Kumleta nyumbani mtoto mgeni inahitaji kumjengea mazoea. Kumleta nyumbani mtoto wa rangi tofauti inaleta changamoto nyingine katika malezi hayo.
Katika mwezi wa kuwaenzi watoto wanaolelewa na watu wengine, karibu zaidi juu ya uzoefu wa watoto weusi ambao kwa kiwango kikubwa hawana uwakilishi wa kutosha katika mfumo wa ustawi wa jamii wa mtoto wa Kimarekani, na hivyo wanalelewa na familia za wazungu.
Changamoto gani ambazo wazazi na watoto hawa wanakutana nazo wakati familia zinapoungana na watu wa rangi tofauti? Nini wale wanaolelewa wanafikiria katika kujiunga na familia hizo, mashule na jamii mbalimbali ambazo hazina mchanganyiko mkubwa wa rangi watu wa rangi mbalimbali?.
ALBUQUERQUE, New Mexico - Kwa zaidi ya miaka 20, Megan Walsh amekuwa anazisaidia familia mbalimbali kukaribisha watoto kulelewa majumbani mwao. Mwanamama huyu amegundua kuwa changamoto huongezeka pale mzazi na mtoto wanapokuwa na rangi tofauti.
“Familia nyingi zinazoamua kuwalea watoto wanahangaika sana wakati wanapowachukua watoto wa rangi tofauti kuwalea kwa sababu hawako tayari kukabiliana na changamoto za malezi kama hayo ya watoto wa rangi tofuati,” Walsh amesema, akisisitiza kuwa wazazi lazima watambue “ wanawataka watoto wao aghlabu kuwa ni tabaka la wachache” katika familia zao na sehemu nyingine.
Walsh alikuwa ni mkurugenzi kwa muda mrefu wa shirika la La Familia- Namaste, ni wakala wa watoto wanolelewa katika makao makuu ya jiji hili kusini magharibi mwa Marekani. La Familia huwasiliana na familia zilizoko tayari kulea kwa ajili ya takriban watoto 80 kila mwaka. Thuluthi ya nafasi hizo za malezi huo ni kwa ajili ya watoto wa rangi tofauti na familia hizo. Walsh alirejea katika jimbo lake alipozaliwa Washington mwaka 2018, na hivi sasa anafanya kazi kama mtaalamu wa afya ya tabia katika kliniki ya kutibu watoto.
Huko Albuquerque, alisaidia familia ya Hill, ambayo binti yao mzaliwa wa Afrika Kusini, Lizelle, hivi sasa akiwa na umri wa miaka 16, anafahamu unajisikiaje unapokuwa “rangi tofuati.”
“Wakati mwengine, ninaingia darasani, na kitu cha kwanza kinacho nikabili katika akili yangu, ‘je, kuna mtu mwengine mweusi katika chumba hiki ambaye ninaweza kujifananisha naye, ambaye anataka kufanana na mimi?” amesema.
Wazazi wa Lizelle ni wazungu, na wakiwa makini, kama alivyonasihiwa na Walsh, kuheshimu tofauti mbalimbali zinazojitokeza za mtoto wakati unajaribu kumjengea hisia ya kuwa ni sehemu ya familia hiyo.
Uelewa huo ndio uliowawezesha Lizelle na mama yake, Deborah Hill, kufika kuanzisha saluni ya nywele na ngozi Kamaria Creations, iliyojikita katika kushughulikia Wamarekani weusi.
“Nyingi ya familia [zenye mchanganyiko wa rangi], kile nilichogundua ni kuwa wanaanza kuja ndani na kuulizia nywele, hicho ndio kitu cha kwanza kinachowaleta – ‘ ninataka kujua jinsi gani ninaweza kuzitunza nywele za mtoto huyu!’” amesema Neema Hanifa, mmiliki wa saluni hiyo.
“Lililo na uzito zaidi,” ameongeza Hanifa. “Ni kuwa na ari, bila ya wasiwasi. Ni vile mtoto anavyojihisi kuwa katika mji kama New Mexico, ambako kuna idadi ndogo ya watu wenye asili ya Kiafrika.
Chini ya asilimia 3 ya watu wa New Mexico wanajitambulisha kama weusi au Wamarekani weusi, kwa mujibu wa takwimu za Sensa iliyofanywa. [[census.gov/quickfacts/NM]]
Hill anasema kupitia binti yake – na pia kupitia mwanawe wa kiume Levi, ambaye alichukuliwa kulelewa baada ya kuzaliwa tu huko Albuquerque ambaye wazazi wake ni wa asili ya Haiti na Kenya --- alikuja kufahamu kuwa “ nywele ni suala la kisiasa ya jamii katika utamaduni wetu.” Sio tu aliweza kugundua saluni kwa ajili ya binti yake, lakini pia amekuwa akidurusu blogi mbalimbali, vitabu na picha za video katiika mtandao wa Youtube staili mbalimbali na jinsi ya kushughulikia nywele za watu weusi.
“Sisi tunayo mafungamano na jamii za watu weusi hapa na katika maeneo mengine ambayo tumewahi kuishi, ikiwemo Afrika,” Hill amesema katika barua pepe. Yeye na mumewe, George Schroeder, wanaamini watoto wao hawatakiwi kukua katika familia zenye wazungu watupu, kwani hilo halitaweza kuchangia katika uzoefu wao wa maisha ya kawaida watakapokuwa wao wenyewe peke yao.
Walsh anafikiria wazazi wanaolea watoto ambao ni weusi wa rangi tofauti ni lazima wawatafute watu wazima weusi ili wawe ni kigezo kwao – madaktari wa watoto ambao ni weusi, waalimu, madaktari wa meno --- na hasa wanapokuwa wanaishi katika maeneo ambayo waliowengi ni wazungu.
“Watafute marafiki na watu ambao ni rangi ya mtoto wao, lakini pia na marafiki wa makabila mengine,” Walsh amesema. “Watoto wanatakiwa kujua kuwa wazazi wao wanaridhia na kuthamini watu wenye utamaduni tofauti na wao na kuwaona ni watu kama wao.”
Ameongeza kusema, “ Kujifunza kuthamini kila mtu wa rangi tofauti na kutokuwa na uwoga wa kile tusichokijua, hili nafikiri ni jambo kwa kweli muhimu. Watu wanaokwama kwa sababu ya upofu wa kutambua watu wa rangi nyingine, nahisi wanawanyima malezi bora watoto wao, kwa sababu hawawafundishi kwamba vile watoto wao walivyo wanapendeza na vipi walikuja ulimwenguni ni muhimu na chachu kwa kila mtu.