Takribani watu 20 wamefariki, 10 wameokolewa baada ya basi kupinduka kwenye mto Mwingi nchini Kenya

Takribani watu 20 wamefariki, 10 wameokolewa baada ya basi kupinduka kwenye mto Mwingi.

Katika video iliyoonekana na gazeti la Star siku ya Jumamosi, basi hilo lilijaribu kuliongoza gari hilo kupita daraja lililofurika maji kwa usaidizi wa wakazi.

Baada ya dakika chache, basi hilo lilionekana likihangaika kusogeza magurudumu yake kwa vile mawimbi ya maji yalikuwa makali sana hivyo kulipeleka mtoni.


Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Mashariki Joseph Yakan alithibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini.

The Standard limeripoti kuwa basi hilo lilikuwa na takriban watu 30, ajali hiyo ilipotokea saa 11 asubuhi katika Kijiji cha Ngune, Mwingi ya Kati.

Polisi walisema wanakwaya hao walikuwa wakielekea kwenye harusi ya mwenzao.

Baadhi ya abiria walionekana wakipiga kelele na kuinua mikono yao kupitia madirishani huku basi hilo likizama taratibu

Mungu azilaze roho za maharehemu mahali pema peponi, Amina

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii