RAIS SAMIA AVUNJA BODI YA TPA NA MSCL.

Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza Wizara kuichukulia hatua Bodi ya Mamunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa madalali badala ya kampuni iliyosajiliwa

Maamuzi ya Rais yanafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda ya kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini

Aidha, Rais ameonesha kusikitishwa kwa Mamlaka kutochukua hatua wakati yapo mambo mengi yaliyoibuliwa na CAG na amemwambia Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kama atashindwa kushughulikia aseme ili amuweke mtu mwingine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii