Utakuta
maelfu ya makala zikielezea jinsi binzari ya manjano zinavyoweza kutibu
magonjwa kama kiungulia, kukosekana kwa uwezo wa tumbo wa kusaga chakula,
kisukari, huzuni na maradhi ya ubongo ya Alzheimer.Inaweze hata kuponya
saratani.
Maelfu ya
tafiti yamekwishafanywa juu ya binzari ya manjano. Kiungo hiki kinasemekana
kuwa na manufaa ya kimatibabu, na kiana kiungo kiitwacho curcumin.
Majaribio
yaliyofanywa kwa panya yameonyesha kuzuia aina nyingi za saratani kukua ndani
yake.
Lakini
binzari manjano huwa na asilimia mbili hadi tatu za curcumin na tunapoila,
miili yetu haifyonzi kiasi chote hicho. Hatahivyo, tafiti kuhusu binzari za
manjano huripoti kwa nadra kiasi cha kawaida cha binzari hiyo katika mlo.
Kwahiyo
ulaji wa kiasi kidogo cha Binzari ya manjano kunaweza kuboredha afya yetu au je
tunapaswa kutumia virutubisho vya binzari ya manjano au curcumin kujikinga na
magonwa.
Kubaini hili, tulitathmini utafiti uliofanywa
Uingereza juu ya athari za kiafya za binzari ya manjano.
Tulianza na utafiti uliofanywa na Chuo kikuu
Newcastle. Watu 100 waliojitolea walifanyiwa majaribio. Watu hawa waligawanywa
katika makundi matatu .
Kundi la kwanza lilipewa kijiko kimoja cha binzari
ya manjano kila siku. Kundi la pili likapewa kiasi hicho hicho cha binzari ya
manjano kama kirutubisho (suplement). Kundi la tatu liliitwa binzari ya manjano
na kupewa kitu kingine.
Tulifanya vipimo vya sampuli za damu. Kipimo cha
kwanza kiliangalia jinsi seli za damu za watu wanaokula binzari ya manjano
inavyokabiliana na magonjwa na ilionyesha ni jinsi gani mfumo wake wa afya
ulikuwa.
Hi inaweza kuelezea iwapo binzari ya manjano inaweza
kupunguza magonwa kiasi cha kuathiri magonjwa ya kudumu kama vile kisukari.
Katika awamu ya tatu ya vipimo, huku seli nyeupe za
damu zikihesabiwa.
Matokeo yalihitajika kwa ajili ya kipimo cha
vinasaba DNA . Lakini tathmini yake pia ilitupatia tathmini wazo la hali ya
mfumo wa kinga ya mwili ya watu waliohusika katika utafiti.Kipimo cha tatu
kilitengenezwa na Chuo kikuu cha London- University College London. Kubadilisha
utendaji wa DNA. Utafiti huu ulifanyika ili kujua vitu vinavyopambana na
saratani vya binzari ya manjano
Hapakuwa na tofauti ya vinasaba katika DNA baina ya
wale waliotumia binzari ya manjano na wale waliotumia virutubisho vya binzari
ya manjano. Lakini wale ambao walitumia binzari ya manjano katika mlo wao
walikuwa na utofauti kwenye muundo wao wa DNA.
.
Ni mapema sana kusema iwapo binzari ina athari
chanya au hasi, lakini binzari ya manjano inaweza kuwa ya faida kwa uundwaji wa
seli zinazofanana na seli alisilia katika utendaji wa jeni.
Binzari ya manjano, pilipili na mafuta kwa pamoja
unaweza kuwa ni mchanganyiko unaoweza kuwa wa manufaa kwa afya.
Hatahivyo ni vigumu kubaini njia ya kupunguza hatari
za kusababisha ugonjwa wa muda mrefu, kama vile saratani (au ugonjwa wa moyo).
Kwahiyo, kipimo chochote ambacho kinaweza kutoa tahadhari sahihi ya mapema wa
magonjwa au zinazoweza kuwa bora vya kutosha kung'amua hata mabadiliko madogo
katika hatari zinazohusiana.