MMOJA AFARIKI, GARI LA ABIRIA LIKITEKETEA KWA MOTO.

Ajali ya magari 4 iliyohusisha malori 3 na basi la abiria kampuni ya classic lenye namba za usajili 68842 Ak 05 imetokea Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe katika Mji wa Mlowo Majira ya saa 4 usiku basi hilo linalofanya safari zake Nchini Tanzania na Congo DRC limeteketea kwa moto huku mtu mmoja akifariki na wengine 18 wakiwa majeruhi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amefika katika eneo hilo la tukio na kutoa taarifa kuwa basi hilo lilikuwa na abiria 13 na wafanyakazi wa basi 6 huku chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na kupaki barabarani kwa lori ambalo lilikuwa linabadilishwa tairi.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii