Serikali imesema Maambukizi mapya kwa Vijana kati ya miaka 15 hadi 24 yamezidi kuongezeka huku Wasichana wakiwa vinara katika janga hilo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, amesema taarifa za utafiti zinaonesha Maambukizi mapya ya VVU yanawakabili zaidi Vijana wenye umri huo na yamefikia 40%, huku 80% kati yao wakiwa Vijana wa Kike
Ameongeza kuwa Mikoa ambayo ina maambukizi makubwa yaliyo juu ya kiwango cha Kitaifa ni Njombe, Iringa, Mbeya, Kagera na Geita. Mikoa yenye kasi kubwa ya maambukizi ni Geita, Simiyu, Manyara na Dododoma.