Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameomba Shirikisho la Soka la Afrika kwa Watu Wenye Ulemavu (FAAF) kuifikiria Tanzania katika kuandaa Kombe la Dunia
Ameomba hayo katika Mkutano Mkuu wa FAAF, ikiwa ni siku chache tangu Timu ya Tanzania ya Tembo Warriors ifuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa Soka la Watu Wenye Ulemavu Nchini Uturuki
Amesema Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa Kombe hilo kwani ina mazingira wezeshi ya kuendesha mashindano makubwa.