Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba wakazi wa Mbagala kuwa watulivu wakati akitatua changamoto zao kwa kile alichokibainisha kuwa amerithi kasi ya ufanyaji kazi.
Pia ameahidi kuifanya Mbagala kuwa wilaya mara tu uchumi wa nchi utakapotengamaa baada ya ugonjwa wa virusi vya korona (Uviko-19) kupungua.
ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 3, 2021 wakati akisalimiana na wakazi wa Mbagala akiwa njiani kuelekea Mkuranga mkoani Pwani.