Rais Donald Trump awasili nchini China

Rais wa China Xi Jinping amempokea mgeni wake Rais wa Marekani Donald Trump nchini humo.

Trump, Xi na Putin wanatarajiwa kuwa na mkutano katika Mji wa Shenzhen kusini mwa China Alhamisi ya juma hili.

Inaelezwa kuwa huenda watatu hao wakazungumzia masuala mbali mbali ikiwemo Ukraine, Ulaya, vita vya Iran, silaha za nyukilia na Taiwan lakini pande hizo hazijawekwa wazi agenda kuu ya mkutano wao.

Awali Rais Xi Jinping na Vladimir Putin walikuwa na mazungumzo kusini mwa China wakati wa kikao na viongozi kutoka nchi 21 wanachama (APEC).

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii