Jeshi la Chad limesema wanamgambo wa Boko Haram wamewaua wanajeshi 23 katika shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi iliyo katika eneo la Ziwa Chad.
Jeshi la Chad lilisema wanamgambo wa Boko Haram wamewaua
wanajeshi 23 katika shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi katika eneo la Ziwa
Chad.
Eneo hilo limekuwa likitishiwa kwa muda mrefu na kundi la
wanamgambo wa Boko Haram lenye makao yake Nigeria, ambalo linajulikana kwa
kufanya mashambulizi katika nchi jirani.
Jeshi la Chad lilisema wanajeshi wengine 26
walijeruhiwa katika shambulio la Jumatatu usiku kwenye kisiwa cha Barka
Tolorom.
Hata hivyo katika taarifa yake ya jana Jumanne jeshi la Chad lilisema idadi kubwa ya wanachama wa kundi la Boko Haram waliangamizwa na washambuliaji hatimaye wakafukuzwa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime