Hapo Aprili 21, 2026 Klabu ya Yanga Sc ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Muungano kwa mwaka 2026/2027 baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi City katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Yanga walionesha ubora wao mapema katika mchezo huo, wakitawala kabisa dhidi ya wapinzani wao na kupata bao la kwanza dakika ya 17 kupitia Prince Dube akimalizia pasi kutoka kwa Allan Okello.
Dakika 34, Frank Assinki aliongeza bao la pili kwa kichwa baada ya mpira wa krosi kutoka kwa Shekhan Khamis, kabla ya Shekhan mwenyewe kufunga bao la tatu dakika ya 38 kwa shuti kali lililomshinda kipa.

Aidha kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama cha kwanza, ambapo Prince Dube alikamilisha ushindi wa Yanga kwa bao lake la pili dakika ya 57, akimalizia pasi safi kutoka kwa Edmund.
Hata hivyo ushindi huo unaendeleza ubabe wa Yanga SC kwenye mashindano ya ndani na kuwapandisha hatua ya nusu fainali wakiwa na morali kubwa kuelekea hatua zinazofuata za Kombe la Muungano.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime