Miili 33 yafukuliwa kutoka kwa kaburi la pamoja Kericho

Nchini Kenya, karibia miili 33 imefukuliwa kutoka katika kaburi la pamoja katika kaunti ya Kericho kwenye mkoa wa bonde la ufa. Watu wawili wakiwa tayari wanashikiliwa na polisi wakuhusishwa na tukio hilo.

Miili hiyo inajumuisha watoto 25 nyengine nane ikiwa ni ya watu wazima kulingana na mamlaka kwenye eneo hilo.

Imeripotiwa kwamba baadhi ya miili hiyo ilikuwa imeanza kuoza wakati nyengine ikiwa bado, ishara kuwa huenda ilizikwa kwa nyakati tofauti.

Tayari miili hiyo imehifadhiwa kwenye makafani kwa uchunguzi zaidi kubaini sababu zilizopelekea izikwe kwenye kaburi la pamoja na ilitoka wapi.

Aidha zoezi la upasuaji linatarajiwa kufanyika kwenye miili hiyo kubaini namna watu hao walivyouawa au chanzo cha vifo vyao. Mwaka wa 2024, miili zaidi ya 400 ilifukuliwa kwenye msitu wa Shakahola kaunti ya Malindi pwani ya Kenya.

Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa watu hao walifariki baada yao kufunga kula chakula wakiwa na imani kwamba wangeenda mbinguni, uchunguzi zaidi ukibaini baadhi ya waliofariki waliuawa kwa kupigwa. Mchungaji wao Paul Mackenzie akiwa bado anashikiliwa na polisi.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii