RC Shigela: Hakuna Mwekezaji Katika Uwanja wa CCM Katoro

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela, ametangaza rasmi kuwa hakuna mwekezaji halali katika eneo la uwanja wa mpira wa CCM Katoro eneo ambalo lilizua taharuki kati ya Serikali ya Kijiji na Chama Cha Mapinduzi.

RC Shigela ametoa kauli hiyo akizungumza na wananchi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro, akieleza kuwa mtu aliyedaiwa kuwekeza katika eneo hilo hakuwa na mikataba wala vibali vya kufanya uwekezaji wowote.

Amesema Serikali imefanya uchunguzi baada ya agizo la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Mheshimiwa Riziki Shemdoe, aliyeagiza taarifa ya kina kuhusu mgogoro huo ndani ya siku 14.

Mhe. Shigela amewataka wananchi kuwa watulivu na kusubiri majibu ya vikao vya ndani baina ya Serikali na Chama, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu atakayevamia mali ya umma bila kufuata utaratibu.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Katoro, Injiniya Kija Limbu Ntemi, amesema wamepokea maelekezo ya Serikali na kupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimamia suala hilo kwa maslahi ya wananchi.

Ikumbukwe Januari 23 mwaka huu Kamati ya Fedha na Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilibaini kuwa mwekezaji tajwa alikuwa akiendelea na shughuli bila vibali, hali iliyosababisha sintofahamu eneo hilo.

Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @georgekivumbi  tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz.


#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii