Mabalozi wa Umoja wa Ulaya wanazidisha juhudi za kumzuia Rais wa Marekani Donald Trump asiwawekee washirika wa Ulaya ushuru mkubwa, wakati wakijitayarisha na hatua za kulipiza kisasi endapo ushuru huo utaongezwa.
Ambapo Januari 17 mwaka huu Trump alitoa onyo kali kwa mataifa kadhaa ya Ulaya huku akitishia kuyaongezea ushuru wa bidhaa endapo Marekani haitaruhusiwa kununua kisiwa cha Greenland.
Hivyo kwa mujibu wa tamko hilo mataifa yanayolengwa ni Denmark, Sweden, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Finland, Norway, na Uingereza huku Mataifa makubwa ya Umoja wa Ulaya yameonakana kukosoa vikali kauli hiyo kwa kuelezea kuwa ni shinikizo na isiyokubalika kidiplomasia.
Kutokana na hali hiyo, viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana mjini Brussels siku ya Alkhamisi katika mkutano wa dharura wa kilele, kujadili hatua za pamoja za kukabiliana na tishio hilo.
Aidha miongoni mwa hatua zinazopendekezwa ni kurejeshwa kwa ushuru wa euro bilioni 93 dhidi ya bidhaa za Marekani, ambao ulikuwa umesitishwa kwa muda wa miezi sita. Endapo uamuzi huo utapitishwa, ushuru huo unaweza kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 6 Februari.
Hata hivyo hatua hizo zinaashiria kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya, huku pande zote zikionyesha msimamo mkali kuhusu maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime