Rais Bernardo Arevalo wa Guatemala ametangaza hali ya hatari ili kukabiliana na magenge yaliyouwa maafisa wanane wa polisi
Ambapo Arevalo alisema kuwa tayali vyombo vya usalama vimerejesha udhibiti wa magereza matatu yaliyokuwa yametwaliwa na magenge hayo mwishoni mwa wiki.
Akitoa hutuba katika taifa hilo usiku wa kuamkia Januari 19 Arevalo alidai kwamba hali hiyo ya hatari itadumu kwa siku 30 ndani ya nchi nzima.
Hatua hiyo ambayo inavisitisha kwa muda baadhi ya vifungu vya katiba, wakati taifa hilo la Amerika ya Kusini likipambana na magenge mawili ya Barrio 18 na Mara Salvatrucha, au M-13.
Hivyo Magenge hayo yanatambuliwa kuwa makundi ya kigaidi nchini Guatemalana Marekani na yanatuhumiwa kwa mauaji ya kupanga, upotezaji watu na biashara ya madawa ya kulevya.
Aidha Mamlaka nchini Guatemala zinayatuhumu magenge hayo kwa mauaji ya polisi wanane siku ya Jumapili (Januari 18) kulipiza kisasi kwa serikali iliyokataa kuwahamishia viongozi wao kwenye gereza lenye kiwango kidogo cha ulinzi.
Hata hivyo Mauaji hayo yalifanyika kwenye mji mkuu wa Guatemala pamoja na maeneo ya karibu, siku moja baada ya wafungwa wenye mafungamano na magenge hayo kuwateka watu 46 kwenye magereza matatu nchi nzima.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime