Viongozi wa Kimataifa Waalikwa Kusimamia Awamu ya Pili ya Makubaliano ya Kusitisha Vita Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary Peter Szijjarto amesema kuwa Waziri Mkuu Viktor Orban amekubali mwaliko wa kujiunga na bodi ya kimataifa itakayokuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa hatua zinazofuata katika makubaliano ya kusitisha vita kwenye Ukanda wa Gaza.

Orban anayejulikana kama mmoja wa waungaji mkono wakubwa wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump barani Ulaya ni miongoni mwa viongozi waliothibitisha ushiriki wao katika bodi hiyo.

Viongozi wengine waliokubali mwaliko huo ni pamoja na To Lam mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Taiwan kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, nchi nyingine zilizotangaza jana kuwa zimepokea mialiko ya kujiunga na bodi hiyo ni India, Australia, Jordan, Cyprus na Pakistan awali, Kanada, Uturuki, Misri, Paraguay, Argentina na Albania zilikuwa tayari zimethibitisha kupokea mialiko kama hiyo.

Bodi hiyo ya kimataifa itakuwa na jukumu la kusimamia awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha vita, ambayo yalianza tarehe 10 Oktoba.

Awamu hii inaelezwa kuwa nyeti na tete ikijumuisha mipango ya kuundwa kwa kamati mpya ya Wapalestina ndani ya Ukanda wa Gaza, kutumwa kwa kikosi cha kimataifa cha ulinzi, kunyang’anywa silaha kundi la Hamas pamoja na kuanza kwa juhudi za ujenzi upya wa Gaza uliosambaratishwa na vita.

Hatua hizi zinaonekana kuwa sehemu ya juhudi pana za kimataifa za kurejesha utulivu wa kudumu katika eneo hilo huku jumuiya ya kimataifa ikifuatilia kwa karibu utekelezaji wake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii