Raia mashariki mwa nchi ya DRC, wameukaribisha mwaka mpya 2026 huku wakiwa hawana chakusherehekea kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama kwenye baadhi ya maeneo ya mashariki ambako waasi wa AFC/M23 wanapigana na vikosi vya Serikali, FARDC.
Kwa wakazi wengi wa mji wa Goma unaokaliwa na waasi hao, hali ya uchumi imezidi kuwa mbaya.
Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, familia nyingi zimeweza kusherehekea mwaka mpya kwa shangwe lakini mwaka huu hali ni tofauti, kama wanavyoelezea wananchi hao.
"Miaka iliyopita hali ya maisha ilikuwa nzuri lakini mwaka huu wa 2025 hali ni ngumu, hakuna pesa kwa hiyo hatujuwe lakufanya ". alisema mmoja wa raia wa mashariki ya Congo.
Katika mji huu wa Goma, baadhi ya familia zimeamua kutosherehekea mwaka mpya kutokana na mzigo wa kiuchumi. Hali hii imesababisha huzuni na wasiwasi miongoni mwa wakazi, ambao wana matumaini ya mabadiliko katika mwaka ujao.
"Ninayo matumaini kwa sababu ni mwenyezi Mungu ndiye anafahamu kitakachotokea na ndiye anayepanga kila kitu maishani, kwetu sisi ilikuwa ni vigumu kuandaaa sherehe sababu hakuna pesa benki zimefungwa na wenzetu wapo kwenye kambi na hivyo kusababisha hali mbaya ya maisha". alieleza raia wa mashariiki ya Congo.
Hata hivyo, wakijitahidi kukabiliana na hali hiyo ya ufukara. Katika maeneo mengine ya mashariki mwa Kongo, changamoto za kiusalama pia zimechangia hali hiyo, ikiwemo ukosefu wa ajira na amani. Hali ya kukwama kwa huduma za benki pia katika mji wa Goma imekuwa na athari kubwa, haswa katika maandalizi ya sherehe za mwisho wa mwaka. Watu wengi wanakumbana na changamoto za kifedha, huku shughuli za kibiashara zikikumbwa na matatizo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime