EU Yasisitiza Greenland Haiwezi Kujadiliwa Bila Denmark

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Antonio Costa amesema kuwa Umoja wa Ulaya utaiunga mkono Greenland na Denmark inapohitajika na hautakubali ukiukaji wa sheria za kimataifa popote pale unapotokea.

 Umoja wa Ulaya (EU) umesema wazi kuwa hakuna uamuzi wowote unaoweza kufanywa kuhusu mustakabali wa Greenland bila kuhusisha Denmark huku ukisisitiza mshikamano wake kamili na watu wa eneo hilo.

Akizungumza katika hotuba ya kuashiria kuanza kwa Cyprus kushika urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya kiongozi wa EU alisema kuwa Greenland ni suala linalohusu Denmark moja kwa moja na akaongeza kuwa wakazi wa kisiwa hicho wana uungwaji mkono kamili wa Umoja wa Ulaya.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump katika siku za hivi karibuni amekuwa akirejea msimamo wake wa kutaka kuichukua Greenland ambapo Trump amedai kuwa kisiwa hicho kina umuhimu mkubwa katika mkakati wa kijeshi wa Marekani na kuishutumu Denmark kwa kushindwa kufanya vya kutosha kukilinda.

Hatan hivyo madai hayo yamezua mjadala na wasiwasi mkubwa katika jumuiya ya kimataifa huku viongozi wa Ulaya wakisisitiza umuhimu wa kuheshimu mamlaka ya nchi na sheria za kimataifa katika masuala yanayohusu ardhi na mipaka ya kitaifa.

  #10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii