Rais Donald Trump, anathmini njia za namna Marekani inavyoweza kuchukua na kudhibiti kisiwa cha Greenland, kinachomilikiwa na Denmark.
Ikulu ya White House imesema, matumizi ya kijeshi ni njia mojawapo inayoweza kutumiwa kudhibiti kisiwa hicho, hali ambayo inazua wasiwasi na uwezekano wa kisiwa hicho kuvamiwa.
Karoline Leavitt, msemaji wa White House amesema, Marekani inahitahi Greenland kwa sababu za kiusalama kaulu ambayo rais Trump amekuwa akisisitiza mara kwa mara hivi karibuni.
Baada ya matukio ya Venezuela ambapo kikosi maalum cha jeshi kilitekeleza operesheni ya kumteka na kumsafirisha Marekani, rais Nicolas Maduro, kuna mashaka kuwa hilo huenda likafanyika kwenye kisiwa hicho kinachopatikana kati ya bahari za Arctic na Atlantic.
Onyo hili la Marekani linakuja, siku chache baada ya uongozi wa Greenland na Denmark kutaka mazungumzo ya haraka na Marekani ili kutatua sintofahamu iliyopo.
Denmark na washirika wake wa Ulaya, wameendelea kusisitiza kuwa Greenland yenye wakaazi 57,000 haiuziki na inasalia ĂȘneo la wenyeji linalomilikuwa na Denmark.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime