Hatimaye Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama na mke wake Michelle
Obama, wametolea ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa kuwa ndoa yao ipo katika
“mgogoro”.
Mapema mwanzao mwa mwaka huu, kulienea taarifa mbali mbali kuwa wawili
hao hawana maelewano mazuri katika ndoa yao, hivyo wanashughulikia suala la
talaka ili kila mmoja aendelee na maisha yake.
Wakitolea ufafanuzi kuhusu suala hilo katika mahojiano ya kipindi
kinachorusha maudhui kwa njia ya mtandao (Podcast) kinachoitwa MO, mbacho
huongozwa na Michelle Obama pamoja kaka yake, Craig Robinson, wanandoa hao
wamesema ni kweli wanafahamu kuhusu uvumi huo, lakini hauna ukweli wowote.
Kwa Upande wake Michelle Obama amesema kuwa, ni kweli kuna changamoto na
magumu ambayo yanajitokeza mara kadhaa kwa, lakini hilo haliwezi kumfanya
aachane na mume wake
“Haijawahi kujitokeza hali yoyote katika ndoa yetu
ambayo imenifanya nifikirie kumuacha mume wangu. Kuna muda tumekuwa tukikutana
na magumu, lakini tumekuwa na mazuri mengi pia. Hiyo imenifanya kuwa mtu bora
kwa sababu ya mwanaume ambaye amenioa” alisema Michelle.
Aidha Barack Obama
aliongeza kuwa, watu wasipowaona pamoja katika matukio mbali mbali, basi huhisi
kuwa wawili hao wanataka kuachana, kitu ambacho sio kweli.