Makumi ya watu wameuawa karibu na kituo cha usambazaji wa misaada kusini Gaza

Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Gaza (GHF) limeripoti vifo 20 katika kituo cha usambazaji wa misaada kusini mwa ardhi ya Palestina siku ya Jumatano, Julai 16, likiwatuhumu watu wenye silaha kwa kusababisha "mkanyagano."

"Kulingana na taarifa zetu, 19 kati ya waathiriwa wamekanyagwa na mwingine alidungwa kisu katika mkanyagano uliosababishwa na ghasia katika umati wa watu," shirika hilo la kibinafsi, linaloungwa mkono na Marekani na Israeli,me katika taarifa.

Wakati huohuo mtaalamu wa Umoja wa Mataifa aliye na dhima ya kufuatilia hali ya mambo kwenye maeneo ya Wapalestina amesema wakati umewadia kwa mataifa kote ulimwengu kukomesha kile amekitaja kuwa "mauaji ya kimbari" ya Ukanda wa Gaza.

Francesca Albanese, anayeshughulikia Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, ametoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka nchi 30 waliokusanyika kwenye mji mkuu wa Colombia, Bogota kujadili vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas.

Wajumbe hao wanatafuta njia ambazo mataifa duniani yanaweza kutumia kukomesha mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Kwenye hotuba yake Albanese amesema nchi duniani zinapaswa kupitia upya ushirikiano wao na Israel na kusitisha mara moja mahusiano na taifa hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii