Timu ya taifa ya Senegal imeshinda ubingwa wa michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya mabingwa mara 7 na wakihistoria timu ya taifa ya Misri kwenye mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Olembe Yaoundé Cameroon.
Timu hizi zilifikia hatua ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kucheza dakika 120 ambazo zilimalizika kwa suluhu 0-0, kwenye penati hizo Sengeali walifunga peanati 4 kati ya 5 walizopiga, Misri walikosa penati 2 kati ya 4 walizopiga hivyo Senegal wakaibuka kwa ushindi wa penati 4-2.
Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Senegal katika fainali 3 walizocheza kwenye nichuano hii ya mataifa barani Afrika, Fainali ya kwanza walicheza mwaka 2002 walifungwa na Cameroon kwa mikwaju ya penati 3-2, na fainali ya pili walicheza mwaka 2019 wakafungwa na Algeria bao 1-0, na jana ilikuwa ni fainali yao ya na tatu na ya pili mfululizo.
Misri ambao ni mabingwa mara 7 na wakihistoria wa michuano ya AFCON wamepoteza fainali yao ya 3 katika fainali 10 walizocheza na mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa michuano hii ilikuwa mwaka 2010 ambapo waliifunga Ghana mabo 1-0 kwenye mchezo wa fainali.
Kwa upande wa tuzo Sadio Mane wa Senegal ametajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano, golikipa wa Senagl Edouard Mendy kipa bora na mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar amemalizi akiwa kinara wa ufungaji akiwa na mabao 8.