LIL YACHTY - NAMUOGOPA NICK MINAJ, HIP-HOP HAIJAFA.

Rapa Lil Yachty amekiri kwamba mpaka sasa bado anajutia maamuzi yake kwa kuchagua upande kwenye vita kati ya Card B na Nick Minaj mwaka 2018 .

Kupitia mahojiano ambayo ameyafanya na Shannon Sharpe kupitia Club Shay Shay rapa huyo kutoka Atlanta ameweka wazi kuhusu namna alivyo jihusisha na mzozo kati ya Card B na Nick Minaj mwaka 2018 na katika vita hiyo alichagua kuwa upande wa Card B jambo ambalo anasema analijutia mpaka sasa kwa sababu lilikua na matokeo hasi kwa kiasi kikubwa.

Mbali na hivo Lil Yachty amekiri kuwa Card B na Nick Minaj wote wanavipaji vikubwa kwenye Muziki.. Licha ya tofauti zao kwake anawaheshimu wote huku akiongeza kuwa yuko na hofu kwenye kumuomba msamaha Nick Minaj kutokana na kilichotokea. 

Kwa upande mwingine Lil Yachty ametoa maoni yake kuhusu mwenendo wa Muziki wa Hip-Hop kwa sasa na kusema kuwa Hip-Hop haijafa kama inavyozungumzwa bali ni nyakati tu kama ilivo kwenye maisha kwamba kuna kupanda na kushuka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii