Nchini Ethiopia, wafugaji wa Afar, kaskazini mashariki mwa nchi, wanakataa kuhamishwa, licha ya hatari ya matetemeko mapya ya ardhi. Tangu mwanzoni mwa mwaka, eneo hili, pamoja na lile la Oromia, limekumbwa na matetemeko kadhaa ya ardhi, muhimu zaidi ambayo, mnamo Januari 4, yalikuwa na ukumbwa wa 5.7 kwenye kipimo cha Richter. Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwahamisha watu 60,000, lakini baadhi yao wanakataa kuondoka.
Kulingana na Uchunguzi wa Jiolojia wa Marekani na Kituo cha Utafiti cha Ujerumani cha Sayansi ya Jiolojia, mitetemeko hiyo husababishwa na magma, mawe yaliyoyeyushwa yaliyo chini kabisa ya ardhi, ambayo hupenya ndani ya udongo, karibu na volkeno mbili. Kwa hivyo, hatari ya matetemeko mapya ya ardhi bado iko juu. Mbaya zaidi, volkano zinaweza pia kulipuka. Lakini hii haitoshi kuwashawishi wafugaji elfu kadhaa kuondoka eneo hili.