Hivi karibuni rapa Cardi B amefunguka kuhusu ushawishi wake kwenye Muziki tangu mwaka 2015 alipoanza kufanya Muziki .
Cardi B amesema hayo wakati akijibia kuhusu watu wanaoponda kwamba hajatoa msaada kwa watu ama hajasaidia wasanii wa kike kuwainua kisanaa.
Card B amesema kuwa label za muziki kwa sasa zina chukua wasanii kwa sababu ya mafanikio yake . Anaendelea kwa kusema kwamba label mbalimbali za muziki duniani haswa Marekani walimpa taarifa kwamba walianza kuchukua wasanii wa kike kwa sababu ya mafanikio yake kwenye Muziki kwa hivo iko ni kigezo tosha kusema kuwa amefungua njia kwa wasanii wengine pia
" Mwanzo ilikua ni ngumu kwa msanii wa kike kupata dili kwenye lebo za muziki bila ya kujali una kipaji kiasi gani, ni mzuri kiasi gani. Ila kupitia Bodak Yellow lebo za Muziki walianza kuamini kwamba unaweza kutengeneza pesa hata kwa wasanii wa kike "
Sio mara ya kwanza kwa Cardi B kuzungumza mchango wake kwenye Muziki. Tangu aanze kufanya Muziki ni wazi kwamba amekua miongoni mwa wasanii wenye mafanikio zaidi kwenye Muziki huu wa kizazi kipya.