Dk. Maduhu" Ipunguzieni Serikali Mzigo wa Kuwahudumia Wafungwa"

Serikali imekiri kubeba mzigo mkubwa wa kuwahudumia wahalifu waliopo magerezani kwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula, malazi na gharama za matibabu huku ikiitaka Idara ya Huduma ya Uangalizi kuielewesha jamii na makundi mbalimbali juu ya umuhimu wa kifungo cha nje ambacho kitaipunguzia serikali mzigo huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Dkt. Maduhu Kazi wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Kazi za Idara ya Uangalizi unaojumuisha Maafisa Probesheni kutoka mikoa 26  sambamba na kuwagawia kompyuta kwa ajili ya kazi zao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii