Marekani yaweka vikwazo zaidi kwa China

Utawala wa Rais Biden, wa Marekani, Jumatatu umetangaza kuweka vikwazo kadhaa vipya kwa bidhaa kwenda China, vikizuia kuuzwa kwa vifaa muhimu vya teknolojia za viwandani, na vile vikubwa vya kuweka kumbukumbu za kompyuta.

Kanuni hizo mpya za marufuku wa mauzo ya vifaa 24 tofauti na program za komyuta tatu, vyote vilivyokuwa vikitumika na kujulikana kama vya teknolojia ya juu, vya haraka, na ufanisi mkubwa katika soko la sekta ya vifaa hivyo.

Marufuku ya mauzo hayo kwenda China, ya idara ya viwanda na usalama chini ya wizara ya biashara ya Marekani, pia inajumuisha kuhamishwa kwa vifaa vya kompyuta vyenye uwezo mkubwa vinavyo husiana na akili mnemba AI.

Wakati huohuo, serekali ya Marekani, imeziongeza kampuni 140 nyingi zikiwa za China, za vifaa vya kompyuta vya viwandani, katika orodha ya watu na makampuni yanayowekewa vikwazo kufanya biadhara.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii