Takriban Mashabiki 56 Wamepoteza Maisha Uwanjani Nchini Guinea

Takriban watu 56 wamepoteza maisha katika msongamano uliotokea kwenye mechi ya soka katika Uwanja wa Stade du 3 Avril, Nzérékoré, nchini Guinea.

Tukio hilo lilianza baada ya mashabiki wa timu ya kigeni ya Labé, kurusha mawe uwanjani kufuatia uamuzi wa mwamuzi wa kutoa kadi nyekundu mbili kwa timu hiyo na penati yenye utata, ndipo polisi walipowatawanya kwa mabomu ya machozi.

Hata hivyo, idadi ya vifo inapingwa na wengi nchini humo wakiamini waliofariki wanafikia watu 100.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii