Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akimshukuru na Kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda kwa namna alivyochagiza shamrashamra za Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.Rais Samia ametoa pongezi hizo kwenye Mkutano wa Wakuu nane wa nchi za EAC wanaokutana Jijini Arusha kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya hiyo.