Taifa la Georgia lasitisha azimio la kujiunga na EU

Chama tawala cha Georgia Alhamisi kimesema kuwa taifa hilo litasitisha mazungumzo kuelelekea kujiunga kwenye Umoja wa Ulaya hadi 2028, huku pia likisusia misaada ya kifedha kutoka Brussels, na kwa hivyo kusimamisha ombi la kujiunga na Umoja huo, hatua ambayo imekuwa lengo lake kwa muda mrefu.

Hatua hiyo ilipelekea maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono kujiunga na EU kuandamana kwenye mji mkuu, wakati rais wa wananchi akilaumu serikali kwa kutangaza vita dhidi ya watu wake. Chama cha Georgian Dream kimetuhumu EU kwamba inatumia matusi, na kupitia taarifa kimesema kuwa inatumia mazungumzo kuelekea kujiunga kwa Georgia kama njia ya kushika mateka Georgia na kupanga mapinduzi ndani ya nchi.

Kimeongeza kusema kuwa, “Kutokana na hilo tumeamua kutoweka kipaumbele suala la kuanza mashauriano na EU hadi mwishoni mwa 2028. Pia tumekataa misaada ya kila aina kutoka Umoja huo hadi mwisho wa 2028. Georgia yenye wakazi milioni 3.7 ina azimio la kujiunga na EU kwenye katiba yake, likiwa taifa lenye kuegemea upande wa Magharibi zaidi miongoni mwa mataifa yaliokuwa chini ya Usovieti.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii