Nyaya za internet zilizoharibiwa nchini ya Bahari ya Baltic zarekebishwa

Moja ya nyaya za kupeleka internet chini ya bahari ya Baltic anayoshukiwa kuharibiwa maksudi mapema mwezi huu imekarabatiwa kulingana na msemaji wa kampuni husika ya Arelion.

Ukarabati wa nyaya hizo zinazounganisha Sweden na Lithuania ulikamilika Alhamisi na mfumo huo umeanza kufanya kazi kikamilifu, msemaji huyo kwa jina la Martin Sjogren ameongeza kusema.

Nyanya zingine mbili za aina hiyo zinazounganisha Finland na Ujerumani ziliharibiwa chini ya saa 24 kati ya Novemba 17-18, na kupelekea waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius kusema kuwa wanashuku ziliharibiwa maksudi. Nyaya za chini ya bahari husafirisha data ya internet kote ulimwenguni na ni kiungo muhimu kwa kuwa zinaunganisha mawasiliano kati ya nchi.

Wachunguzi wanashuku kwamba ziliharibiwa na meli kubwa ya mizigo cha China ya Yi Peng 3, wakati waziri mkuu wa Sweden Ulf Kristersson akisema kuwa nchi yake imetuma ombi rasmi kwa China la ushirikiano kuhusu kilichopelekea uharibifu huo chini ya maji ya bahari ya Baltic. Msemaji wa kampuni iliofanya ukarabati Martin Sjogren amesema kuwa wanashirikiana na polisi wa Sweden kwenye uchunguzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii