Siku mbili baada ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kutoa rai kwa vijana nchini Kenya kupigania haki zao na utawala bora nchini Kenya, Rais William Ruto amemtuhumu mtangulizi wake huyo kuwachochea vijana nchini Kenya kufanya fujo.
Usemi huo wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta umezua taharuki nchini Kenya, Rais William Ruto akijibu usemi wa mtangulizi wake Kenyatta amewataka viongozi kukoma kuwachochea vijana kufanya fujo na badala yake kuwatafutia nafasi bora za ajira.
Wakati hayo yakijiri aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, amefichua kuwa analenga kuunda Muungano wa kisiasa pamoja na viongozi wengine nchini Kenya kwa lengo la kuingia Ikulu mwaka wa 2027.