Asilimia moja ya raia wa Sudan Kusini, sasa wana umeme, baada ya serikali kuanza kutekeleza mkakati wa kusambaza nishati hiyo kwa maendeleo ya wananchi wa taifa hilo.
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya nishati Sultan Lam Tungwar wiki hii amesema hatua hiyo ni mpango wa muda mrefu kuhakikisha kuwa raia wa nchi hiyo Milioni 11 wanauganishwa na umeme kwa kuanza kuwekeza kwenye ujenzi wa mabwawa.
‘‘Asilimia moja ya watu wa Sudan Kusini wana umeme lakini asilimia 99 ya wananchi hao kamwe hawana umeme. Sasa tunamulika hali hii kwa makini. Lengo letu kubwa ni kupata umeme kutoka Uganda. Ni biashara kwani bwawa la Karuma nchini Uganda liko tayari kutupatia umeme. Hivi karibuni tutakuwa na nguvu za umeme ambao utasambaa kote nchini.’’ AmesemaNaibu Katibu Mkuu katika Wizara ya nishati Sultan Lam Tungwar.