Askari Polisi wapewa darasa changamoto Afya ya akili

Askari Polisi Mkoani Iringa wametakiwa kujiepusha na vitendo vinavyopelekea tatizo la afya ya akili na kwamba inapotokea miongoni mwao kuonekana na tatizo hilo apatiwe msaada wa haraka, ili kuepusha madhara zaidi.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Polycarp Urio wa Makao Makuu ya Polisi Dodoma, wakati akitoa elimu hiyo kwa Maafisa na Askari na kusema tatizo hilo limekuwa likiongezeka hali iliyopelekea kufanyika kwa jitihada ili kunusuru hali hiyo.

Kwa upande wake Msaikolojia kutoka Kitengo cha Ushauri Nasihi Makao Makuu ya Polisi, Konstebo Omari amewasisitiza Askari kutafuta msaada wa haraka pale anapohisi kuwa na changamoto za afya ya akili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii