Russia imekataa kuthibitisha kama Korea Kaskazini inaisaidia

Russia ilikataa kuthibitisha mipango yake kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini ambao inasemekana inapanga kupeleka katika mapambano yake dhidi ya Ukraine, wakati wa makabiliano na Marekani Jumatatu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

“Nilisikia taarifa ya mjumbe wa Russia, kama walivyofanya wengine katika kikaoiki, lakini swali linabaki kuwa taarifa haijibu, kama kuna wanajeshi wa Korea Kaskazini, waliopo Russia,” Naibu wa balozi wa Umoja wa Mataifa, Robert Wood aliwaambia wajumbe wa baraza hilo.

Wood alikuwa akizungumzia taarifa za kijasusi zinazoonyesha kuwa takriban wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini wamepelekwa Russia, kwa mafunzo na kupigana pamoja na wanajeshi wa Kremlin nchini Ukraine, huku baadhi ya Wakorea Kaskazini wakiaminika kuelekea Ukraine katika siku zijazo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii