Tanzania imetajwa kuwa kati ya mataifa 10 bora barani Afrika ambayo yana miundombinu bora zaidi ya barabara.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwa imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kuanzia mijini hadi vijijini.
Uwekezaji huo unalenga kuwarahisishia wananchi, kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo usafirishaji kwa urahisi ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mtandao wa Statista huku ikichapishwa na businessinsider, Tanzania katika 10 bora hizo ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 4.41 huku Namibia ikishika nafasi ya kwanza.