Rais wa Iran, asema kusimamishwa mapigano kutaathiri muitikio wao

Rais wa Iran, Jumapili amesema uwezekano wa kusimamishwa mapigano baina ya washirika wake na Israel, kunaweza kuathiri kiwango cha mwitikio wa Tehran, kwa mashambulizi ya karibuni ya Israel katika maeneo ya kijeshi ya Iran.

Kama Israel, inatafakari tabia yake, kukubali kusimamisha mapigano na kuacha kuua watu wanaokandamizwa na wasio na hatia katika ukanda, kutaweza kuathiri kiwango na namna ya mwitikio wetu, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, amesema akinukuliwa na shirika la habari la serekali IRNA.

Ameongeza kwamba Iran, haitokaa bila kujibu uchokozi wowote dhidi ya himaya na usalama wake kwa mujibu wa shirika la habari.

Ndege za Israel, zilifanya mashambulizi Oktoba 26 katika kile Israel, inasema ni kujibu mashambulizi ya Tehran ya Oktoba 1.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii