Maafisa wa jeshi la Cameroon wamesema kwamba wanafanya uchunguzi baada ya video iliyosambazwa mitandaoni ikionyesha mwimbaji maarufu akiteswa na vikosi vya usalama.
Maafisa wa jeshi la Cameroon walisema siku ya Alhamisi kwamba wanafanya uchunguzi baada ya video iliyosambazwa mitandaoni ikionyesha mwimbaji maarufu akiteswa na vikosi vya usalama.
Video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionekana ikionyesha msanii huyo wa muziki kwa jina kamili Longkana Agno Simon anayejulikana pia kama Longue Longue, akiteswa wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ilisema katika taarifa.
Ilisema mwimbaji huyo alishutumu kikosi maalum cha ulinzi wa kijeshi kwa kutekeleza dhulma hiyo.
Mwimbaji huyo maarufu wa mtindo wa Makossa wa Cameroon amemkosoa Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 91, ambaye ametawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 41.