Ufaransa itatoa euro milioni 100 kwa Lebanoni, atangaza Emmanuel Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kwamba Ufaransa itatoa euro milioni 100 kwa Lebanoni, akiongeza kwamba "vita vinapaswa kukoma haraka iwezekanavyo" kati ya Israel na Hezbollah.

"Ufaransa itatoa msaada wa euro milioni 100", ametangaza siku ya Alhamisi rais wa Ufaransa katika ufunguzi wa mkutano kuhusu Lebanoni ambao unalenga kukusanya takriban euro milioni 500 kusaidia watu waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo. "Vita vinapaswa kukoma haraka iwezekanavyo," ameongeza Emmanuel Macron, akibainisha kuwa lengo ni "kuthibitisha uhuru wa Lebanoni", kwa hiyo "kuonyesha kwamba mbaya zaidi haijaandikwa na kuruhusu Walebanoni kurejesha udhibiti wa hatima yao.

Berlin inatoa euro milioni 96 kusaidia Lebanoni

Serikali ya Ujerumani imeahidi "kutoa jumla ya euro milioni 96 za ziada ili kukabiliana na mzozo wa Lebanoni" wakati wa mkutano wa kimataifa huko Paris siku ya Alhamisi.

"Lengo ni kufikia wakimbizi wa ndani na kuhakikisha uthabiti wa kijamii, kiuchumi na kitaasisi nchini Lebanoni," zimeandika, katika taarifa ya pamoja, Wizara za Mambo ya Nje na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi ambazo zimtoa kiasi hiki cha jumla.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii