China imeshikilia msimamo wake kwa kumalizwa kwa vita vya Ukraine kwa njia ya amani.Hatua ya China imekuja baada ya Marekani kuipa Ukraine ruhusa ya kutumia makombora ya masafa marefu dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Urusi.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya kigeni wa Beijing Lin Jian, amewaambia wanahabari kwamba usitishaji wa mapigano na suluhu la kisiasa itakuwa muhimu kwa pande zote kwenye mzozo huo.
China imekuwa ikisisitiza kwamba haiegemei upande wowote wa mzozo wa Ukraine na kwamba haitoi usaidizi wa kijeshi kwa upande wowote kama inavyofanya Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.
Licha ya kutangaza kutochukua upande kwenye mzozo huo, China imesalia kuwa mshirika wa karibu wa kisiasa na kiuchumi wa Urusi.
Mataifa wanachama wa NATO wameituhumu Beijing kwa kuisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine na hatua yake ya kukosa kulaani uvamizi wa Urusi.
Beijing imeongeza kwamba itaendelea kutumia mchango wake katika kuhakikisha suluhu inapatikana.