Zaidi ya asilimia 91 ya wapiga kura wameidhinisha katiba mpya katika kura ya maoni iliyofanyika Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Gabon Hermann Immongault amesema katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa.
Waliojitokeza walikadiriwa kuwa asilimia 53.5 taarifa yake iliongeza kusema. Matokeo ya mwisho yatatangazwa na Mahakama ya Katiba, waziri wa mambo ya ndani amesema.
Rasimu ya katiba, ambayo inapendekeza mabadiliko makubwa ya kimamlaka ilihitaji zaidi ya 50 ya kura zilizopigwa ili kupitishwa.