Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi anazuru Tehran ambapo amekutana na maafisa wa Iran siku ya Alhamisi Novemba 14 kujadili mpango wa nyuklia wa Iran, wiki chache kabla ya kuwasili kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House.
"Azimio lolote la uingiliaji kati (la IAEA) katika masuala ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litakabiliwa na hatua za mara moja," amesema Bw. Eslami wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran pamoja na mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi.
Iran haitafanya mazungumzo "chini ya shinikizo na vitisho" juu ya mpango wake wa nyuklia, mkuu wa diplomasia ya Iran Abbas Araghchi alisema mapema baada ya mkutano huko Tehran na mkuu wa IAEA Rafael Grossi.
"Tuko tayari kujadiliana kwa misingi ya maslahi yetu ya kitaifa na haki zetu zisizoweza kuondolewa, lakini hatuko tayari kujadiliana kwa shinikizo na vitisho," Bw. Araghchi ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.