Rais Samia Amteua Mhandisi Peter Rudolf Ulanga kuwa Mkurugenzi ATCL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Peter Rudolf Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Mhandisi Ulanga anachukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.

Vilevile taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka viongozi imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Prof. Harun Jeremia Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe, anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii