Jamaa Akiri Kumuua Mpenziwe, na Kuuficha Mwili Kwenye Balcony kwa Miaka 16

 Polisi wamemkamata mwanamume anayehusishwa na mauaji ya mpenzi wake miaka 16 iliyopita katika kusini mwa mji wa Geoje  Korea Kusini.

Mwanamume huyo, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 50, alikiri kumuua mpenzi wake na kuzika mwili wake kwenye balcony ya nyumba ya yake. 

Kulingana na ripoti iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Mkoa wa Gyeongnam na Kituo cha Polisi cha Geoje, mwanamume huyo alimpiga mwanamke huyo akitumia kifaa butu na kisha kuuweka mwili wake kwenye begi kubwa la kusafiria.

Mshukiwa aliwaambia polisi kwamba alikuwa akiishi na mwanamke huyo kwa takriban miaka mitano mjini Geoje kabla ya kutofautiana mnamo Oktoba 2008, na kumfanya ampige na kifaa butu. Kisha akauficha mwili huo kwenye balcony yake akiufunika na matofali na kumiminia saruji ya sentimita 10 (inchi nne). Polisi wanasema aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa miaka minane zaidi, kabla ya kukamatwa kwa tuhuma za dawa za kulevya mwaka wa 2016.

Wakati wa uchunguzi wa watu waliopotea mwaka 2011, mwanamume huyo aliwaambia polisi kuwa waikuwa "wameachana" na mpenzi wake hivyo kesi hiyo ilikosa kuamuliwa kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Polisi wanasema aliendelea kuishi katika ghorofa hiyo kwa miaka minane zaidi, kabla ya kukamatwa kwa tuhuma za dawa za kulevya mwaka wa 2016.

Mwili huo ulipatikana mwezi uliopita baada ya mfanyakazi aliyekuwa akitafuta maji yalikokuwa yakivuja kupata begi la kusafiria. Baada ya ukaguzi, polisi walipata mwili wa mwanamke huyo "umehifadhiwa kwa kiasi fulani" lakini mwanamke huyo alitambuliwa vyema kwa kutumia alama za vidole. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii