Mazishi ya Ibrahim Aqil na Ahmad Mahmoud Wehbi, wote makamanda wakuu wa Hizbullah, waliouawa Ijumaa hii katika shambulio la Israel, yamefanyika siku ya Jumapili mchana, katika viunga vya kusini mwa Beirut, ngome ya "Chama cha Mwenyezi Mungu" mbele ya maelfu ya watu. Maandamano ya nguvu kutoka kwa chama cha Kishia na njia ya kuonyesha kwamba licha ya hasara kubwa iliyopatikana wiki hii na mashambulizi dhidi yavifaa vya mawasiliano, azimio lake bado lipo.
Kama ishara ya kupinga Israeli, umati wa maelfu ya wafuasi wa Hezbollah walikusanyika mbele ya jeneza la Ibrahim Aqil na Ahmad Mahmoud Wehbi, makamanda wawili wakuu wa tawi la kijeshi la "Chama cha Mwenyezi Mungu", anaripoti mwandishi wetu huko Beirut Sophie Guignon. Katikati ya barabara ilifurika umati wa watu, wabunge, waziri na hasa Naïm Kassem, nambari mbili wa kundi hilo alizungumza.
"Suluhu la kijeshi la Israel halitawarudisha waliokimbia makazi yao kutoka kaskazini hadi makwao na kutatua tatizo lao. Ili kufanya hivyo, watalazimika kwenda Gaza na kusimamisha vita. Vitisho havitutishi. Na hatuogopi hali mbaya zaidi. Tumeingia katika awamu mpya ya vita,” amesema.
Awamu mpya ambayo inaweza kuwa tayari imeanza kwa shambulio la kwanza la Hezbollah katika maeneo ya kijeshi huko Haifa, nchini Israel. Wakiwa wamejawa na hasira, wafuasi wa Hezbollah wamefunga safu nyuma ya kiongozi wao asiyepingwa Hassan Nasrallah. "Tuko pamoja na upinzani wa Kiislamu, tunafuata maamuzi ya Hassan Nasrallah," anasema Hassan Moqtad, mfuasi wa Hezbollah, katika umati huo. "Inatoa nguvu zaidi, na kile kilichotokea jana usiku ni mwanzo tu wa jibu," anaongeza Ali Zrek, mwenye umri wa miaka 73.
Kuongezeka huku kwa mivutano kwa vyovyote vile kunazua hofu ya kutokea vita kamili nchini Lebanoni. Jeshi la Israel siku ya Jumatatu liliwashauri raia wa Lebanoni "kujiepusha na maeneo yanyolengwa" ya Hezbollah kusini mwa Lebanoni, na kuongeza kuwa mashambulizi yanayolengakundi hilo "yataendelea katika siku za usoni" na kwamba haya yatakuwa "makubwa zaidi na sahihi zaidi".
Wakati huo huo, utafutaji unaendelea kutafuta miili katika vifusi vya jengo lililolengwa na shambulio la Israel siku ya Ijumaa katika viunga vya kusini mwa Beirut. Waokoaji wana shughuli nyingi, umbali wa mita kadhaa, familia zinasubiri kupatikana kwa miili hiyozikiwa na huzuni mkubwa.