Polisi yachunguza mauaji ya Mjasiriamali Moro

Polisi Mkoani Morogoro imesema inafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya Mjasiriamali mkazi wa Maseyu, Costa Clemence (22), lililotokea katika kijiii cha Gwata, Wilaya ya Morogoro.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Alex Mkama imeeleza kuwa tukio hilo lilibainika Septemba 15, 2024 eneo la maseyu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika eneo la tukio halina makazi ya watu na  mwili ulikuwa umetelekezwa na pembeni yake kukiwa na pikipiki isiyokuwa na namba za usajili inayosadikiwa kuwa ni mali ya marehemu.

“Jeshi la polisi linatoa wito kwa wakazi wanaoishi jirani na maeneo hayo na yeyote mwenye taarifa kuhusiana na tukio hilo kuwasilisha kwa Polisi ili kuwakamata waliohusika na mauaji hayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii