Hatua zilizochukuliwa na serikali ya Marekani ni pamoja na vikwazo dhidi ya viongozi wa RT, shirika la habari la serikali ambalo lililazimishwa na wizara ya sheria kusajiliwa kama chombo cha kigeni, na kuwekewa vikwazo vya visa.
Mashirika ya kijasusi hapo awali yalidai kuwa Russia, ilitumia taarifa potofu kuingilia uchaguzi.
Lakini tangazo linalotarajiwa kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland linatarajiwa kuonyesha kwa kina wasiwasi wa Marekani na kuashiria hatua za kisheria dhidi ya wale wanaoshukiwa kuhusika.